Mjane wa Papa Shirandula,awalaumu madaktari wa Karen Hospital kwa utepetevu

Posted by Aldo Pusey on Tuesday, September 24, 2024

-Mke wa Papa Shirandula alisema mume wake alipimwa ugonjwa moja pekee badala ya tatu

-Alisema huenda marehemu alikuwa na changamoto nyingine kiafya kwa sababu COVID-19 yaweza kudhibitiwa

-Ebbie Andega alifichua alikuwa amewaagiza madaktari wampime nimonia na malaria lakini walizingatia COVID-19 pekee

-Mjane huyo aliongeza kuwa aliwaagiza madaktari kumuwekea Papa mashine ya kumsaidia kupumua lakini alikata roho katika sehemu ya kuegesha magari ya hospitali hiyo

Huku Wakenya wakimuomboleza Papa Shirandula, ambaye ni maarufu katika ulingo wa uchekeshaji, mke wake Ebbie Andega bado anashtuliwa na kifo cha mume wake mpendwa,

Mama huyo wa watoto aliwakashifumadkatari wa Hospitali ya Karen kwa utepetevu huku akishilia mume wake angekuwa hai endapo wangezingatia kwa makini dalili zake.

Habari Nyingine: Biwi la simanzi muigizaji maarufu Papa Shirandula akizwa Busia

Habari Nyingine: Seneta Johnson Sakaja aingia chini ya maji huku akisakwa na maafisa wa polisi

Wakati wa karamu ya mazishi ya Papa gatuzini Busia siku ya Jumatatu, Julai 20, mjane huyo akiwa mwingi wa uchungu alisema marehemu alikata roho katika sehemu ya kuegesha magari ya hospitali hiyo na hakuwa amelazwa.

“Alikufa akiwa kwenye kiti cha gari karibu na mimi.Hata hawakumlaza. Tulienda kwenye idara ya kuwalaza wagonjwa ya Karen Hospital na utaratibu ulikuwa na utata. Niliwaagiza wamuweke kwenye mashine kwa sababu ilikuwa suala la dharura lakini hawakufanya hivyo," alisema mama huyo.

Alisema nguli huyo alipimwa ugonjwa wa COVID-19 pekee wakati alikimbizwa hospitalini.

Habari Nyingine: Bintiye Waziri wa Maji Sicily Kariuki, Wendy Muthoni aaga dunia

Ebbie aliongezea kuwa madaktari walipuuza kumfanyia vipimo vingine viwili muhimu (malaria na numonia) ambavyo vingesaidia katika kuokoa maisha ya mume wake.

Mjane huyo anaamini kuwa msimu wa baridi ni hatari kwa mapafu ya watu na huenda mume wake alikuwa anaugua ugonjwa mwingine pia.

“COVID-19 yaweza kudhibitiwa. Papa alitakiwa kufanyiwa vipimo tatu, virusi vya corona, numonia na malaria. Wakati niliwauliza madaktari endapo walifanya vipimo hivyo, walisema hapana. Niliwauliza mbona walizingatia COVID-19 pekee na huenda alikuwa akiugua ugonjwa mwingine," alisema mjane huyo.

Shemeji yake Rowland Wanyama alisema muigizaji huyo alianza kuugua baada ya kutoka kwa ziara yake katika Kaunti ya Kakamega.

Aligunduliwa kuwa na COVID-19 na kukubaliana na madaktari kuwa atarejea nyumbani na kujitenga.

Hata hivyo, wiki moja baadaye Papa alikumbana na matatizo ya kupumua na alikimbizwa katika Hospitali ya Karen Hospital na mke wake Ebbie.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdja4ZyhJJmpKOZnpp6uK2MqZipmV2otaq%2BwKebrqSRlsSiuMCupK5lnZaxorfTmqmiZaeWeqyt0Z6lZqCfqL2qwMClZKSvkWLCtbHPnquerqVjtbW5yw%3D%3D